Carmel Secondary School, yapata Maji ya Uhakika.

Carmel Secondary School ni shule inayojali kuwa na mazingira rafiki na salama kwa mwanafunzi kupata elimu bora.

Elimu ya Carmel Secondary School inamsaidia mwanafunzi kuwa mbunifu na mwenye hekima na mwenye kuyatawala mazingira yanayo mzunguka. Moja kati ya jambo muhimu katika maendeleo ya eneo lolote katika jamii, ni upatikanaji wa maji safi na yenye uhakika kwa mda wote.

Ingawaje kwa mda mrefu Carmel Secomdry School kulikuwa na maji chumvi ambapo uongozi wa shule ukishirikiana na wazazi na wanafuzi, uliazimia kuwa na maji safi na salama kwa afya ya mtumiaji

Hatimaye sasa ndoto yetu imekuwa halisi chini ya usimamizi wa Fr. Simon Rupoli, ambaye amekuwa mstari wa mbele  kuhakikisha upatikanaji wa maji safi kwa matumizi ya shughuli mbalimbali za shule ikiwa ni pamoja na bustani na usafi wa mazingira na mtu binafsi.

Similar Posts

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *